KUMTUMIKIA MUNGU
MAMBO YATAKAYO KUSAIDIA KUMTUMIKIA MUNGU.
1-Nguvu ya Roho mtakatifu
Roho mtakatifu ni ahadi kwa kila mwamini ambayo Yesu alimwahidia mwanadamu.(Yohana16:7-16)
Roho mtakatifu hukaa kwa watu walio amini ya kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yao na kubatwiza. Lakini pia tunaona Yesu anawaagiza wanafunzi wake wasitoke Yerusalemu waingoje ahadi ya Baba ambayo ndiye Roho myakatifu .
Mungu hapo mwanzo aliwapa watumishi wake Roho mtakatifu kulingana na kazi ambayo anataka ifanyike. Roho mtakatifu alikaa na manabii tunaona Nabii kama Eliya Mungu alimpaka mafuta kupitia Roho mtakatifu ambeya alimwongozo katika kutumika pamoja na Mungu.
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
- Roho mtakatifu hutuosha dhambi zetu . Biblia inasema Yohana alibatiza kwa maji lakini Yesu atawabatiza kwa Roho mtakatifu. Ndo maana Roho mtakatifu hukaa na watu walio wasafi wa moyo na yeye hujuza matendo mema. Matendo 1:5,mathayo3:1-12
- Roho mtakatifu hufanya kanisa kuongezeka kupitia ushudiaji. Ukitumika pamoja Roho mtakatifu yeye ndo atafanya ushudiaji ndani ya mioyo ya watu. (matendo2:37-42)
- Roho mtakatifu hutupa ujasiri katika kumtumikia Mungu. Roho mtakatifu alimpa ujasiri Petro kunena maneno ya Mungu baada ya kupata Roho mtakatifu (Matendo1:8)
- Roho mtakatifu hutupaka mafuta. Roho mtakatifu hutupa mafuta kwa ajili ya kutumika kama Mungu alivowapaka mafuta watumishi wake katika agano la kale.( Luka3:21-23)
- Roho mtakatifu hutupa umoja. Matendo2:43-47. Roho mtakatifu hutupa umoja wa kimungu maana yeye ni Mungu. Kanisa linalo ongozwa na Roho mtakatifu ni kanisa lenye upendo na ushirika mzuri.
- Roho mtakatifu hutuongoza. (Matendo19:6 ), Jifunze kumtumia Roho mtakatifu kwa kusikliza sauti yake na kuitambua Roho mtakatifu hutuonya mara kwa mara likini tumeshindwa kutafsiri.
- Roho mtakatifu hutupa maono. (Matendo2:16-18,Yoeli2:28-32)Mungu anasema itakuwa siku mwisho nitamwagia watubwote Roho yangu na wana wenu wataona maono na wezee wenu wataota ndoto.
No comments:
Post a Comment