Monday, November 9, 2020

KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU

 KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU

1:1UUMBAJI WA MWANADAMU

Kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu lilikuwa mwanadamu Atawale vitu vyote Duniani. Ambapo Mungu alimwamuru mwanadamu ale wanyama na kila kitu alichokifanya Duniani. Lakini piah Mungu alitaka mwanadamu amsifu na kumwadu. mwanadamu ilimpasa kumtumikia Mungu akilinda vitu vyake alivofinya kwa mkono wake duniani.

 Biblia inasema  Mungu alipomuumba mtu bado miche ya kondeni wala mboga ya kondeni ilikuwa haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu alikuwa bado hajainyeshea nchi mvua wala hapana mtu wakuilima aridhi.Basi Mungu alipanda Bustani upande wa mashariki ya Edeni akumweka mwanadamu humo.mwanzo2:4-10

Mungu alimuumba mtu mfano wake mwenyeww ambeye wa kwanza mwanamume aliitwa Adamu na wa pili alitoko ubavuni mwa Adamu ambaye alikuwa mwanamke aliitwa Hawa. Wote hawa wawili walikuwa wakiishi katika bustani ya Edeni.Mwanzo2:2125  Lakini Bwana Mungu alimwagiza mtu akisema  matunda yote utayala isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya usiyale wala usiyaguse maana siku utakapokula hakika utakufa.mwanzo2:16-17


MWANADAMU KUONDOKA KWENYE  KUSUDI LA MUNGU

Biblia inasema basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia Hawa ati Mungu ndo alivosema msile matunda ya miti ya bustani?. Mwanamke akamjibu nyoka, matunda ya miti yote twaweza kula isipokuwa matunda ya mti wa katikati Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa.

Nyoka akamjibu mwanamke hakika hamtakufa ,kwa maana Mungu anajua kwamba mkiyala hayo matunda mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya. Mwanzo3:1-5

JAMBO LA KUJIFUNZA

Usimruhusu shetani ukampa nafasi ya kuzungumaza kama Hawa alipomruhusu nyoka kusema naye. Usitoe siri zako wewe na Mungu kwa kila mtu kama Hawa alipo eleza mambo yake yeye na Mungu na kumpa ibilisi shetani nafasi.

Wengi wetu tumeshindwa kujizui kuongea mambo yetu ya siri hata tumempa ibilisi nafasi kujua mambo yetu.Basi tambua kwamba unapotoa siri zako kwa rafiki zako huwezi jua undani wake hata kama unasali nae. Unaweza ukajikuta unakumbana na matatizo na vita isiyo isha kulingana na kuumpa ibilisi nafasi na kutambua kusudi la Mungu kwako. 

MADHARA YA KUONDOKA KATIKA KUSUDI LA MUNGU

 Laana                                                       Mtu alilaaniwa na Mungu na Mungu baada ya kutoka kwenye kusudi lake Bwana Mungu.   Kwamba Mungu alimwambia umelaaniwa kuliko wanyama wote wa mwitu. Mwanzo 3:13-19

LAANA ni hali ya kukataliwa, mtu asiye na kibari  mbele za watu na Mungu piah.                                    

 KUNA NINI KATIKA LAANA

-Huleta maadui kuongezeka juu yako.

- Aridhi itakukataa wala hutaona mafanikio katika maisha yako. mwanzo4:12

-Utakuwa ni mtu asiyekuwa na makao duniani. Mwanzo4:14

-Utakuwa ni mtu aliye hesabiwa kifo. Mwanzo 3:19

-Ni  mtu asiyekubarika na watu kila akuonae hutapata kibali mbele yake. Mwanzo 4:14.     


MAMBO YA KUFANYA ILI UFIKIE KUSUDI LA MUNGU

  • Kutenga mda wa kusoma neno la Mungu . Ili kujua nini Mungu anakusudi gani kwako,lazima uwe mtu wa neno.Yoshua 1:8
  • Ni lazima tuachane na kweli za dunia.kweli za dunia ni kweli alizotumia shetani kumdanganya Hawa kwamba hautakufa ila utajua mema na mbaya. Jambo hili lilimkosesha Hawa Kuishi katika kusudi la Mungu.                                            

-Mfano wa kweli za dunia.

-Mbona unajitengatenga na wezio itakuwa kama mtu asiye na mahusiano muzuri utaone kana  kama unashida

-Ukiwa na mke mmoja utapata baadhi ya magonjwa ya kiume.(tezi dume)

-Binti au kijana usipotongoza au kutongozwa wewe utakuwa na matatizo.

Hizo ni kweli za duniani wala sio kusudi la Mungu.

  • Kutenga mda wa Maombi ,ni vizuri kuwa na mda wa kumuomba Mungu . Bibliabinasema kesheni mkiomba msije mkaingia majaribuni Luka 22:40-46
  • Lazima  umjue na kumwamini unayemtumikia na kumwelewa viđź‘€zuri.Yohana 14:10.

Mungu wa mbinguni akubariki


Sunday, November 8, 2020

KUMTUMIKIA MUNGU

 KUMTUMIKIA MUNGU 

MAMBO YATAKAYO KUSAIDIA KUMTUMIKIA MUNGU. 

1-Nguvu ya Roho mtakatifu

Roho mtakatifu ni ahadi kwa kila mwamini ambayo Yesu alimwahidia mwanadamu.(Yohana16:7-16)

 Roho mtakatifu hukaa kwa watu walio amini ya kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yao na kubatwiza.         Lakini pia tunaona Yesu anawaagiza wanafunzi wake wasitoke Yerusalemu waingoje ahadi ya Baba ambayo ndiye Roho myakatifu .

Mungu hapo mwanzo aliwapa watumishi wake Roho mtakatifu kulingana na kazi ambayo anataka ifanyike. Roho mtakatifu alikaa na manabii  tunaona Nabii kama Eliya Mungu  alimpaka mafuta kupitia Roho mtakatifu ambeya alimwongozo katika kutumika pamoja na Mungu.

KAZI ZA ROHO MTAKATIFU 

  • Roho mtakatifu hutuosha dhambi zetu .  Biblia inasema Yohana alibatiza kwa maji lakini Yesu atawabatiza kwa Roho mtakatifu. Ndo maana Roho mtakatifu hukaa na watu walio wasafi wa moyo na yeye hujuza matendo mema.      Matendo 1:5,mathayo3:1-12 
  • Roho mtakatifu hufanya kanisa kuongezeka kupitia ushudiaji. Ukitumika pamoja Roho mtakatifu yeye ndo atafanya ushudiaji ndani ya mioyo ya watu. (matendo2:37-42)
  • Roho mtakatifu hutupa ujasiri katika kumtumikia Mungu. Roho mtakatifu alimpa ujasiri Petro kunena maneno ya Mungu baada ya kupata Roho mtakatifu (Matendo1:8)
  • Roho mtakatifu hutupaka mafuta.    Roho mtakatifu hutupa mafuta kwa ajili ya kutumika kama Mungu alivowapaka mafuta watumishi wake katika agano la kale.(    Luka3:21-23)
  • Roho mtakatifu hutupa umoja.   Matendo2:43-47.      Roho mtakatifu hutupa umoja wa kimungu maana yeye ni Mungu. Kanisa linalo ongozwa na Roho mtakatifu ni kanisa lenye upendo na ushirika mzuri.
  • Roho mtakatifu hutuongoza.  (Matendo19:6 ), Jifunze kumtumia Roho mtakatifu kwa kusikliza sauti yake na kuitambua Roho mtakatifu hutuonya mara kwa mara likini tumeshindwa kutafsiri.
  • Roho mtakatifu hutupa maono. (Matendo2:16-18,Yoeli2:28-32)Mungu anasema itakuwa siku mwisho nitamwagia watubwote Roho yangu na wana wenu wataona maono na wezee wenu wataota ndoto.

KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU

  KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU 1:1UUMBAJI WA MWANADAMU Kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu lilikuwa mwanadamu Atawale vitu vyote Duniani. Am...