KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU
1:1UUMBAJI WA MWANADAMU
Kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu lilikuwa mwanadamu Atawale vitu vyote Duniani. Ambapo Mungu alimwamuru mwanadamu ale wanyama na kila kitu alichokifanya Duniani. Lakini piah Mungu alitaka mwanadamu amsifu na kumwadu. mwanadamu ilimpasa kumtumikia Mungu akilinda vitu vyake alivofinya kwa mkono wake duniani.
Biblia inasema Mungu alipomuumba mtu bado miche ya kondeni wala mboga ya kondeni ilikuwa haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu alikuwa bado hajainyeshea nchi mvua wala hapana mtu wakuilima aridhi.Basi Mungu alipanda Bustani upande wa mashariki ya Edeni akumweka mwanadamu humo.mwanzo2:4-10
Mungu alimuumba mtu mfano wake mwenyeww ambeye wa kwanza mwanamume aliitwa Adamu na wa pili alitoko ubavuni mwa Adamu ambaye alikuwa mwanamke aliitwa Hawa. Wote hawa wawili walikuwa wakiishi katika bustani ya Edeni.Mwanzo2:2125 Lakini Bwana Mungu alimwagiza mtu akisema matunda yote utayala isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya usiyale wala usiyaguse maana siku utakapokula hakika utakufa.mwanzo2:16-17
MWANADAMU KUONDOKA KWENYE KUSUDI LA MUNGU
Biblia inasema basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia Hawa ati Mungu ndo alivosema msile matunda ya miti ya bustani?. Mwanamke akamjibu nyoka, matunda ya miti yote twaweza kula isipokuwa matunda ya mti wa katikati Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa.
Nyoka akamjibu mwanamke hakika hamtakufa ,kwa maana Mungu anajua kwamba mkiyala hayo matunda mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya. Mwanzo3:1-5
JAMBO LA KUJIFUNZA
Usimruhusu shetani ukampa nafasi ya kuzungumaza kama Hawa alipomruhusu nyoka kusema naye. Usitoe siri zako wewe na Mungu kwa kila mtu kama Hawa alipo eleza mambo yake yeye na Mungu na kumpa ibilisi shetani nafasi.
Wengi wetu tumeshindwa kujizui kuongea mambo yetu ya siri hata tumempa ibilisi nafasi kujua mambo yetu.Basi tambua kwamba unapotoa siri zako kwa rafiki zako huwezi jua undani wake hata kama unasali nae. Unaweza ukajikuta unakumbana na matatizo na vita isiyo isha kulingana na kuumpa ibilisi nafasi na kutambua kusudi la Mungu kwako.
MADHARA YA KUONDOKA KATIKA KUSUDI LA MUNGU
Laana Mtu alilaaniwa na Mungu na Mungu baada ya kutoka kwenye kusudi lake Bwana Mungu. Kwamba Mungu alimwambia umelaaniwa kuliko wanyama wote wa mwitu. Mwanzo 3:13-19
LAANA ni hali ya kukataliwa, mtu asiye na kibari mbele za watu na Mungu piah.
KUNA NINI KATIKA LAANA
-Huleta maadui kuongezeka juu yako.
- Aridhi itakukataa wala hutaona mafanikio katika maisha yako. mwanzo4:12
-Utakuwa ni mtu asiyekuwa na makao duniani. Mwanzo4:14
-Utakuwa ni mtu aliye hesabiwa kifo. Mwanzo 3:19
-Ni mtu asiyekubarika na watu kila akuonae hutapata kibali mbele yake. Mwanzo 4:14.
MAMBO YA KUFANYA ILI UFIKIE KUSUDI LA MUNGU
- Kutenga mda wa kusoma neno la Mungu . Ili kujua nini Mungu anakusudi gani kwako,lazima uwe mtu wa neno.Yoshua 1:8
- Ni lazima tuachane na kweli za dunia.kweli za dunia ni kweli alizotumia shetani kumdanganya Hawa kwamba hautakufa ila utajua mema na mbaya. Jambo hili lilimkosesha Hawa Kuishi katika kusudi la Mungu.
-Mfano wa kweli za dunia.
-Mbona unajitengatenga na wezio itakuwa kama mtu asiye na mahusiano muzuri utaone kana kama unashida
-Ukiwa na mke mmoja utapata baadhi ya magonjwa ya kiume.(tezi dume)
-Binti au kijana usipotongoza au kutongozwa wewe utakuwa na matatizo.
Hizo ni kweli za duniani wala sio kusudi la Mungu.
- Kutenga mda wa Maombi ,ni vizuri kuwa na mda wa kumuomba Mungu . Bibliabinasema kesheni mkiomba msije mkaingia majaribuni Luka 22:40-46
- Lazima umjue na kumwamini unayemtumikia na kumwelewa vi👀zuri.Yohana 14:10.
Mungu wa mbinguni akubariki
No comments:
Post a Comment