Saturday, November 7, 2020

KUMTUMIKIA MUNGU

KARIBU TUENDELEE NA SOMO LETU (katika umtumikia Mungu)

 Tumeona hapo mwanzo nini maana ya kumtumikia Mungu, likini sasa lazima utambue pia kwamba kuna gharama katika kumtumkia huyu Munngu. Tunamwona Yesu mwenyewe alivo pata shida katika kueleza kusudi lake la kuja duniani /naweza kusema kueneza injili kwa wana wa israeli. Ambalo lilikuwa kusudi kila mwanadamu apate injili kama hivi leo.

 Ukisoma biblia( Mathayo 13:54-58) Tunaona Yesu alivopata shida kueneza injili katika nchi yake mwenyewe ambapo watu walimtumbua Yesu kama mtoto wa selemala na waliitambua vyema familia yake Yesu hata hawakuamini mafundisho yake  wala kazi zake inasemekana hakufanya miujiza mingi katika nchi yake mwenyewe watu wengi wa kwenu hawata kuamini.

Kuna watu unaweza kutana nao wanajua injili kuliko wewe,wanaijua biblia sana lakini hawatambui nini maana ya wokuvu ni watu wa dini tu.Tunamwona Yesu alikutana na watu walioshika dini tangu kwa mababu zao wanazijua sheria sana. Lakini Yesu anasema ni watu walioyoshika mapokeo ya wanadamu(Marko 7:1-7)(mstari wa saba unasema  nao waniabudu bure,wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu).

Basi ukitaka kumtumikia Mungu lazima ujikane mwenyewe na kujitwika msalaba wako mwenyewe. Haijalishi ni magumu gani utakumbana nayo utapitia taabu mbalimbali ukizani Mungu amekuacha lakini usikate tamaa Mungu yu pamoja nawe. 

 Tuchukue mfano wa biblia Yohana alifungwa gerezani na Yesu alikuwa akifufua watu na viweta walitembea na vipofu kuona lakini mtumishi wa Mungu Yohana alikuwa amefungwa gerezani wala asifanye muujiza kwake wa kumtoa gerezani(Mathayo11:1-7).

Tunaona hata Yohana mwenyewe anatuma wanafunzi wake wamfuate Yesu na kumuuliza ni wewe masihi ama tumtarajie mwingine ,Yesu anajibu mwambieni vipofu wanona viwete wanatembea, kwanini basi hakumtoa gerezani . Kumbe ilimpasa mtumishi wa Mungu Yohana afe kuwa ushuda wa kutumika pamoja na Mungu, kwamba imetupasa mateso kwa ajili ya watu wengine ili waokolewe. 

Kumbuka:

Kumtumikia Mungu kunahitaji 

1-Uwe msafi wa moyo nikimaanisha kwamba uvae drii ya haki kifuani mwako. Drii ya haki ni kuwa mtakatifu ili uombapo haja zako mbele za Mungu zisikike na zijibiwe piah.(waefeso6:14)

Wengi wetu tumejichanganya katika mambo yetu wenyewe kwa kutegemea akili zetu wenyewe huku tukisubiri kijibiwa haja zetu hali kwamba wajua siri za moyo wako.

2-Uwe mwaminifu ;Mda mwingi tumekosa uaminifu mbele za Mungu na mbele za rafiki zetu lakini kumbuka mwanadamu mwenzio hakuoni lakini Mungu anakutazama kwa jicho la karibu sana, ( maana biblia inasema macho yake Mungu yapo duniani kuwangalia watenda mema na mabaya).

3-Uwe mtu wa ibada ; naweza kusema mshumaa wawezaja kusimama wenyewe bila kuwekewa kishikizo. Mti wawezaje kusimama bila mizizi  ndivo na wokovu lazima uwe na sehemu ya kujishikiza .Nilazima uwe mtu wa sehemu ya ushirika ili uweze kusima. Biblia inasema imani chanzo chake ni kusikia kumbe nilizima kuwa mtu unayependa kusikia maneno ya Mungu. Tunaona ushirika wa kanisa la mitume wa Yesu walivofanya mambo kwa ushirka na kwa upendo walifanikiwa sana!!( Matendo 2:42,)

Tumeona watu wengi wanaokoka ni baada ya kupata ushuda ambao unawajengea imani ndani yao ya kwamba Mungu yupo na anaweza.

4-Lakini pia ni lazima uwe mtu mwenye ushuda mzuri mbela za watu au jamii inayokuzungu ili wakunenee mema na mambo ya hekima yaje kwako. 

Sio mtu unaye sifika kwa mambo ya giza kama uzinzi mtu wa masengenyo mtu watabia za kubeba wake za watu mtu wa kubeba waume za watu mtu wa kubeba binti za watu. Wasikuambie twende tukafanye ushudiaji mtaani kwako ni mtu umejaa hofu ya maovu yako unayoganya huko umeifanya kazi ya Mungu ngumu.Tengeneza ushuda mzuri watu wakutambue.

5-Jambo la tano ni kumtambua unaye mtumikia.  Maran wakristo tumefanya mambo kwa mazoea kanakwamba Mungu ni jamaa mmoja tu hivi tunayemfahamu lakini sio kwamba ni Mungu ambaye anapaswa kusujudiwa.

Napenda nikwambie kwamba mtambue Mungu kama ni mfalme katika maisha yako yote maana biblia inasema ni Mungu aliye na kiti cha ufalme mbinguni . Inatupasa kumweshimu Mungu kwa kumsujudia. 

MUNGU ANASEMA YEYE NI MUNGU MWENYE WIVU NA OLE WAKE ALITAJAYE JINA LAKE BURE

KUTOKA 20:7(Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako,maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure). 

Wengi ni wahubiri wakubwa lakini tumelitaja jina lake Mungu bure! 

Hayo ni mambo machache ya kuyajua ili ili Mungu akutumie katika maisha yako, Tamani kumtumikia Mungu ili awe karibu na wewe. Wengi tumeshindwa kuwa na kiu ya kumtafuta Mungu ndo maana hatuja muona Mungu katika maisha yetu. Mungu anataka watu walio na kiu ya kuutafuta uso wake ili awaonyeshe ukuu wake!! 

KUNA  MAMBO MENGI YAMETUNGE NA USO WA MUNGU

1-Tamaa ,tamaaa ni adui wa haki katika maisha yetu hasa kwa mkristo ni jambo kubwa ambalo limetukosesha sana kumwona Mungu.                                Kwanza kabisa ni: Usinzi ,Fedha . (Waefeso5:3-5).

  • Wengi wetu tumetamani kuwa na vitu vingi vizuri mwanamke mzuri , magari, majumba mazuri. Lakini kumbuka kwamba kuvipata vitu hivi ndo kunaongeza tamaa kwa mwanadamu tunamwona sulemani alipopata mali nyingi ilimpa  kiburiya kuoa wanawake wengi ambapo pia ilipelekea kumweka mbali na uso wa Mungu .     Yote ni kwasababu yalimpelkea kuenenda katika njia zake mwenyenyewe na kuabudu sanamu (1wafalme11:1-7).

Lakini pia Yakobo anasema Mungu hamjaribu mtu maana yeye hawezi kujaribiwa na maovu ,lakini tunajiletea majaribu wenyewe kwa tamaa zetu huku tukivutwa na kudanganywa(Yakobo1:12-16).

2-Maisha ya kidunia ,wengi wetu tumesumbukia maisha yetu wenyewe kuliko mambo ya Mungu. Ndo maana hatujamuona Mungu akifanya kwetu na mda mwingi tumekuwa watu wa kulalamika kila wakati.(Mathayo6:25-34).   Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu hayo Mengine mtazidishiwa. 


Usisite kutoa maoni kwenye box hapo chini . Lakini piah somo nimwendelezo nakuomba jitahidi tumalize   pamoja mimi  nakuombea akupe Mungu akupe ufahamu uzidi kuyapambambanua haya!

 Ubarikiwe na BWANA.

KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU

  KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU 1:1UUMBAJI WA MWANADAMU Kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu lilikuwa mwanadamu Atawale vitu vyote Duniani. Am...