UJIO WA YESU KRISTO ULIMWENGUNI
Kumtumikiia Munguni kushiriki mateso pamoja na Yesu kristo pale msalabani. Kuzaliwa kwa Yesu kusudi ni kumtoa mwadamu katika maisha ya kale maisha ya dhambi. Kifo cha Yesu kilidhihilisha ukombozi kwa mwanadamu kwamba Yesu alikufa na kufufuka siku ya tatu na anasema yeye ukimkubali ukanywa damu yake na na kula mwili wake utaupata uzima wa milele. ( Yesu hakumaanisha kwamba umle yeye naunywe damu yake bali alitaka umkubali yeye kwamba ametumwa na baba ulimwenguni kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu ).Lakini piah kifo cha Yesu kinatupa uhakika kwamba kufa kwetu ni kuishi kwetu kwamba Yesu alifufuka basi nasi siku ajapo Yesu tutafufulia na kuishi tena tena katika makazi mapya ambayo ni Yerusalemu mpya.
Ilimpasa Yesu afe ili kuokoa wengine , kwamba ilipasa Barabara afunguliwe ili Yesu asulubiwe msalabani( Marko15:6-15) . Pia Yesu alimwambia Petro akesama nenda nyuma shetani maana huyawazi ya Mungu ila ya wanadamu, kwa maana petro alitamani Yesu asife abaki pamoja nao lakini huo haukuwa mpango wa Mungu, Yesu kubaki na wanadamu,(Marko 8:33).
Lakini piah kuja kwa Yesu na kuondoka kuna tupa sisi kazi ya kufanya kama alipo waagizi wanafunzi wake ama mitume wa Yesu kwamba amewaachia mamlaka ya kuponya wagonjwa na kila atakaye kula kitu cha kufisha na kung'atwa na nyoka hatadhulika ,Marko 16:14-20.
Lakini pia anasema aliacha vipawa kwa wanadamu pale alipo paa kwenda mbinguni ambapo aliacha wengine kuwa
1-walimu
2-mitume
3-wainjilisti
4-manabii
5-wachungaji
Yote ni ili kuujenga mwili wa kristo Yesu . Kumbe inatupasa kuifanya kazi ya Mungu katika maisha yetu yote ili kutimiza ujio wa Yesu ulimwenguni. Inatupasa kuihubiri injili ya Yesu kwa kila kiumbe na kubatiza kama agizo la Yesu kwa mitume pale Yerusalemu.
Ameni
ReplyDelete